Na Athumani Adam
Nani aliyeamini kwamba Yanga watapata ushindi wa magoli mengi kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania bara kwenye uwanja wa katiba kule Bukoba? Kagera Sugar ni miongoni mwa timu za ligi kuu Vodacom ambazo zina historia ya kutumia vizuri uwanja wa nyumabni.
Kwenye mechi dhidi ya Yanga, mambo yalikuwa tofauti kwa upande wa wenyeji Kagera Sugar.
Japokuwa walianza mchezo vizuri kwa kupata goli la mapema dakika ya tatu kwa shuti maridhawa nje ya 18 lakini hadi kipindi cha kwanza kinaisha tayari Donald Ngoma, Obrey Chirwa na Msuva waliifanya Yanga kuwa mbele kwa mabao 3-1 baada ya kutumia makosa ya mlinda mlango wa Kagera Hussein Sharif ‘Casillas’.
Kipindi cha pili Kagera walipata tena goli la mapema lakini golikipa David Buruani aliyeingia kuchukua nafasi ya Hussein Sharif nae akaruhusu goli tatu hatimae mechi ikaisha kwa Yanga kuibuka na ushindi wa magoli 6-2.
Mbali na matokeo, timu zote zilicheza vizuri, soka la kushambulina kwa kasi. Kuna kipindi Kagera walijaribu kurudi mchezoni hususan kipindi cha pili baada ya kupata goli la mapema dakika za mwanzoni za kipindi hicho na matokeo kusimama 2-3 kwa muda wa dakika kadhaa za mchezo.
Kila timu ilicheza soka la chini kwa muda mwingi wa mchezo, lakini kina George Kavila walizidiwa na viungo wa Yanga Kamusoko na Haruna Niyonzima.
Hali ya uwanja kwa mara ya kwanza iliruhusu mpira kuchezwa kwa staili ile, pasi zilifika kwa walengwa bila kupotea kama ilivyokuwa Kaitaba ya zamani. Nyasi Bandia (artificial Turf) ambazo zimewekwa kwenye uwanja wa Kaitaba kupitia mradi wa FIFA (goal project) zimechangia sana timu kucheza soka lao.
Kila mpira ulipoamrishwa nao ukatiii nilimkumbuka rais aliyekifungoni Sepp Blatter na mradi wake wa goal Project ambapo kila nchin mwanachama wa FIFA anapatiwa dola laki tano za kiamrekani kwa mwaka.
Wakati mwingine tunashindwa kuona soka asilia kwenye viwanja vya mikoani kutokana na uchakavu wa viwanja. Fikiria tu matokeo yangekuwaje kama Yanga wangecheza na Kagera kwenye Kaitaba ya zamani.
Kumbuka tu Kagera walivyokuwa wanacheza kwenye Kaitaba ya zamani dhidi ya Kaitaba ya sasa ambayo imeboreshwa kwa kuwekewa nyasi bandia.
Yawezekana Yanga walishinda mchezo kwa sababu ya mbinu za kiufundi za mwalimu Hans Plujim lakini ubora wa kaitaba ulichangia kupata matokeo
Viwanja vizuri zitanichangia kuona mpira mzuri, shukrani kwa Blatter kwa hisani yake goal Project.

Post a Comment